Friday, May 18, 2012

Lagos,Nigeria amezaliwa mtoto ambae ameshikilia kitabu cha dini yani Quran..mama Kikelomo Ilori (32), alijifungua Jumatatu iliyopita mtoto aliyekuwa ameshikilia Kurani ndogo baada ya kubeba mimba kwa miezi 10 na kwamba licha ya mumewe kumshawishi kuitoa mimba hiyo, alikataa.

“Nilipokataa kutoa mimba, mume wangu alinitelekeza akidai kuwa ‘hilo ni tatizo lako,’ lakini nesi aliyenizalisha alishangazwa na tukio hilo, akasema Kurani itupwe lakini nilikataa, nikasema mama yangu lazima aione,” alisema Kikelomo.

Mchungaji wa kanisa analoabudia mwanamke huyo, Victoria Yetunde Dada alisema wakati wa ujauzito, Kikelomo alikuwa akifika kanisani mara kwa mara kuomba na akamshauri asiitoe mimba hiyo kwa kuwa kiumbe hicho kimeletwa na Mungu.

SOURCE BY TEEN TZ!

No comments:

Post a Comment